Ernest Walton
Kutoka Wikipedia
Ernest Walton (6 Oktoba, 1903 – 25 Juni, 1995) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ireland. Hasa alichunguza mwendo wa vijipande vya atomu. Mwaka wa 1951, pamoja na John Douglas Cockcroft alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.