Web Analytics

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Elimu - Wikipedia

Elimu

Kutoka Wikipedia

Darasa la kijerumani, takriban mwaka wa 1930.
Darasa la kijerumani, takriban mwaka wa 1930.

Elimu ni mojawapo ya sayansi jamii. Inagusa vipengele vya kufundisha, kujifunza, ujuzi maalumu, mawazo na ustadi. Walimu wanatumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kufundisha mtalaa. Mambo hayo yanaelezwa katika majarida na vitabu vingi vya mada za elimu. Fasihi hiyo inataja aina tofauti za utekelezaji wa mafunzo unaotumia masomo, michezo, mitihani, mipango ya wakati, hamasa, mitambo mbalimbali kama kompyuta na kadhalika. Hata hivyo, kipengele muhimu kabisa ni uhusiano kati ya wanafunzi na tabia ya mwalimu. Sifa za uhusiano huo zinaweza kuwahamasisha wanafunzi wajifunze kwelikweli. Walimu bora wanawasiliana utathmini mwema, uzoefu na busara jinsi wanafunzi watavutiwa. Walimu wakiweza kufahamu wanafunzi kwa ndani, kuondoa dhuluma na ubaguzi, kuunda hali ya kufundishika na kutambua uwezekano uliopo, watawawezesha wanafunzi wawe na matarajio makubwa zaidi kwao wenyewe na kwa jamii kwa jumla. Lengo la elimu ni kuwasaidia wanafunzi wawe wanajamii wanaofaa katika jamii inayoendelea. Kila kizazi wajifunze utamaduni wao (angalia uendeshaji umma) ili wakomae na kutambua wajibu wao pamoja na mahitaji katika jamii ya ulimwengu inayozidi kutofautika.

Yaliyomo

[hariri] Jumla

Imetambulika na kukubaliwa na wengi kwamba elimu inaanza mtu azaliwapo na kuendelea wakati wa maisha yake yote. Wengine wanaamini kuwa elimu inaanza hata mapema zaidi kama wazazi wanaomwimbia au kumsomea mtoto tumboni wakitumai la kwamba mawasiliano hayo yatamsaidia katika maendeleo yake.

Mara nyingi watu wanamaanisha elimu rasmi tu lakini kila aina ya uzoefu unaojenga ufahamu ni sehemu ya elimu yetu, iwe darasani, iwe katika maisha ya kila siku.

Kila mtu hupata elimu isiyo rasmi kutoka vyanzo mbalimbali. Elimu ya mtu inasaidiwa sana na familia yake, na siku hizi vyombo vya habari vinaiathiri pia.

[hariri] Istilahi

Neno la elimu ni neno kopo kutoka Kiarabu.

[hariri] Falsafa ya elimu

Lengo la falsafa ya elimu ni kutafiti na kuelewa madhumuni, asili, kanuni na mifano kamilifu ya elimu. Mada nyingine ni ufahamu wenyewe, asili ya akili, shida za mamlaka ya mwalimu, uhusiano kati ya elimu na jamii na kadhalika. Tangu wakati wa Rousseau falsafa ya elimu imehusishwa na nadharia za saikolojia na maendeleo ya binadamu.

Kusudi la msingi la elimu ni lifuatalo: Mafanikio ya jamii yoyote yanategemea kuwaelimisha vijana wawe raia wanaowajibika, wanaofikiria na walio na ujasiri wa kuendesha umma. Ni jukumu lenye changamoto linalohitaji ufahamu wa ndani wa maadili, nadharia ya siasa, ujumi na uchumi. Pia lazima kuelewa tabia na haki za watoto, kwao wenyewe na katika jamii.

[hariri] Asili ya ufahamu

Kwa kawaida, lengo la elimu ni kupasha mtu ufahamu. Elimu ya ufahamu pia huitwa epistemolojia. Somo hilo linachunguza asili ya ufahamu na uhusiano wake na ukweli na mawazo. Ni lazima kwa wanafunzi kuunganisha maarifa mapya na maarifa ambayo wameshayajua ili kujifunza na kuelewa. Katika ukuaji wa ufahamu elimu inagusa mada kama maarifa, ujuzi, busara na utambuzi nafsia.

[hariri] Saikolojia ya elimu

Saikolojia ya elimu ni somo la jinsi wanadamu wanavyojifunza. Pia huchunguza kufaa kwa elimu katika mazingira fulani, saikolojia ya kufundisha, na saikolojia za asasi za kielimu.

[hariri] Masomo ya kitaalamu

Masomo ya kitaalamu ni matawi ya ufahamu ambayo hufundishwa kwenye chuo kikuu. Mifano ya masomo hayo ni sayansi asili, sayansi umbile, hisabati, sayansi jamii, na sayansi tumizi. Kila somo lina masomo mengine ndani yake, k.m. ndani ya sayansi umbile kuna fizikia na kemia, au ndani ya sayansi jamii kuna saikolojia, siasa na kadhalika.

[hariri] Elimu rasmi

Elimu rasmi inatokea ikiwa kuna mtalaa ulioundwa kwa ajili ya kuwaelimisha watu.

[hariri] Historia

Mwaka wa 1994, Dieter Lenzen, mwenyekiti wa Chuo Kikuu Huru cha Berlin, alisema kwamba "elimu ilianza ama mamilioni ya miaka yaliyopita ama mwisho mwa mwaka wa 1770". Lenzen alitaka kuonyesha kuwa elimu kama sayansi jamii haiwezekani kutengwa na mapokezi ya kielimu yaliyotangulia. Uprofesa wa ufundishaji wa kwanza ulianzishwa mwaka wa 1770 kwenye Chuo Kikuu cha Halle, Ujerumani.

Kwa ajili ya maendeleo ya jamii ni lazima kwa watu wazima kuwaelimisha watoto wao. Katika jamii isiyo na uandishi, watu walikuwa hupasha ufahamu kwa mdomo na kwa mifano. Baadaye, maandiko (yawe ishara, yawe herufi) yamesaidia kudumisha ujuzi.

Baada ya kupanua ujuzi wa jamii zaidi ya ustadi wa msingi kama mawasiliano, biashara, kuhifadhi vyakula na kadhalika, ufundishaji na elimu rasmi zilikuwa hufuata. Ufundishaji wa aina hiyo ulikuwepo kule Misri kati ya miaka 3000 na 500 KK.

[hariri] Ulaya

Katika nchi za Ulaya elimu iliathiriwa na mashirika ya dini: Mapadre na watawa walitambua umuhimu wa kupasha ufahamu, nao walianzisha shule. Vyuo vikuu vingi vya Ulaya vimeanzishwa na Kanisa la kikatoliki.

Wakati wa Uongofu (Enlightenment) uhusiano kati ya elimu na dini ulisahauliwa. Jean-Jacques Rousseau alifanya utafiti katika maendeleo ya akili ya mtoto.

Mwaka wa 1773, Muungano wa Poland na Lithuania waliunda Tume ya Elimu ya Taifa (kwa Kipoland: Komisja Edukacji Narodowej, kwa Kilithuania: Nacionaline Edukacine Komisija) inayohesabika kama Wizara ya Elimu ya kwanza katika historia ya binadamu.

[hariri] Uchina

Katika nchi ya Uchina, elimu ilianza na maandiko ya serikali, siyo ya kidini. Kwa ajili ya kuwaelimisha wafanyakazi wao, Mfalme Mkuu wa Uchina alianzisha mfumo wa mitihani ya kitaifa kati ya mwaka wa 206 KK na wa 220 BK. Mfumo huo uliendelea mpaka mwaka wa 1911 ulipobadilishwa kufuata mfumo wa elimu kutoka Ulaya.

[hariri] Japani

Katika nchi ya Japani, elimu ilianza na dini ya Ubudha.

[hariri] Uhindi

Nchi ya Uhindi ina historia ndefu ya elimu rasmi. Mfumo wa Gurukul wa elimu ni mojawapo wa mifumo ya kwanza duniani. Wanafunzi walipata mafunzo katika dini ya Kihindu, falsafa, maandiko ya Kisanskriti, upigaji vita, siasa, uganga wa Ayurveda na historia.

[hariri] Elimu duniani kwa kisasa

Katika miaka iliyopita hali ya kutokujua kusoma wala kuandika imepungua sana. Kwa mfano idadi ya watu wasiokwenda shuleni ilipungua kutoka asilimia 36 katika mwaka wa 1960 kwenda asilimia 25 katika mwaka wa 2000.

[hariri] Marejeo

  • Brief review of world socio-demographic trends shows world illiteracy trends.
  • Dubois, H.F.W., Padovano G. & Stew, G. (2006) Improving international nurse training: an American–Italian case study. International Nursing Review 53(2): 110–116.
  • Lucas, J. L., Blazek, M. A., & Raley, A. B. (2005). The lack of representation of educational psychology and school psychology in introductory psychology textbooks. Educational Psychology, 25, 347-351.

[hariri] Viungo vya nje

Static Wikipedia (no images)

aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -

Static Wikipedia 2007 (no images)

aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -

Static Wikipedia 2006 (no images)

aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu

Static Wikipedia February 2008 (no images)

aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu