Ambwene Yessayah
Kutoka Wikipedia
Ambwene Allen Yessayah (amezaliwa tar. 5 Julai, 1981, Mtwara) ni mwanamuziki wa muziki aina ya Komesho, Rap na Hip Hop, Muigizaji na pia mwanamitindo kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina la AY. AY Ametoa nyimbo nyingi maarufu nchini Tanzania, moja kati ya nyimbo hizo kama vile Raha tu 1-2, Raha Kamili, Machoni kama watu, Binadamu nk.
AY ambaye anafahamika sana nchini Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi hadi Kusini mwa Afrika. Vile vile Alikuwa member wa kundi la East Coast Team linaloongozwa na Gwamaka kaihula alimaarufu kama King Crazy GK kabala ya yeye4 na mwenzake khamis mwinjuma maarufu kama mwana Falsafa au Mwana FA, ambaye zaidi yeye anapenda aitwe FA au Binamu kuondoka katika kundi hilo la Muziki lenmye maskani yao Upanga jijini Dar es salaam