Aime Cesaire
Kutoka Wikipedia
Aimé Fernand David Césaire (25 Juni 1913 - 17 Aprili 2008) alikuwa mshairi, mwandishi na mwanasiasa Mfaransa mwenye asili ya Kiafrika kutoka kisiwa cha Martinique katika Bahari ya Karibi.
Pamoja na Léopold Sédar Senghor na Léon-Gontran Damas alianzisha dhana ya negritude. Alikuwa mwalimu wa Frantz Fanon.
Baada ya kupita nafasizote za elimu kisiwani Martinique alipewa nafasi ya kusoma huko Ufaransa kuanza 1931. Masomoni alikutana na Leopold Senghor wakawa marafiki. 1939 alirudi Martinique akawa mwalimu shuleni akimfundisha Frantz Fanon. Kabla ya kurudi aliandika shairi kubwa yenye urefu wa kitabu "Cahier d'un retour au pays natal" (daftari ya kurudi kwenye nchi nilikozaliwa).
1945 alichaguliwa kuwa meya wa Fort-de-France na mbunge katika bunge la Ufaransa huko Paris wa msaada wa chama cha kikomunisti. Bungeni alipeleka sheria iliyotaka kuzipa koloni hali ya mikoa ya Ufaransa. Baada ya uvanizi kwa Hungaria na jeshi la Umoja wa Kisovyeti aliachana na Wakomunisti.
Aliendelea kuwakilisha Martinique bungeni hadi 1993. Kwake kisiwani alikuwa mwenykiti wa bunge la mkoa kati ya 1983 na 1988. 2001 alijiuzulu katika siasa.
Kiwanja cha Ndege cha Martinique ilipewa jina la "Martinique Aimé Césaire International Airport" kwa heshima yake tar. 15 Januari 2007.
[hariri] Matamshi
- Juu ya ukoloni
Mkoloni anayemwangalia mwanadamu mwenzake kama mnyama ili kutuliza dhamira yake huyu mkoloni atageukia kuwa mnyama mwenyewe. - Naambiwa habari za maendeleo na magonjwa yaliyoponywa lakini mimi naongea juu ya tamaduni zilikanyagwa na watu maelfu waliokandamizwa. Nonaongea juu ya watu mamilioni waliofundishwa kutetemeka, kupiga magoti, kukata tamaa.
- Juu ya umoja wa watu wote
Hakuna mbari ambao pekee yake una uzuri, akili, nguvu; kwa wote kuna nafasi kwenye mkutano wa washindi