Tambi
Kutoka Wikipedia
Tambi ni chakula kinachotengenezwa kutoka kwa kinyunga cha unga na maji kuwa kama milia membamba inayopikwa katika maji au supu. Ni chakula muhimu katika nchi nyingi hasa Italia, China, Japani na Korea. Siku hizi zimeenea kote duniani. Aina zinazoliwa sana kimataifa ni pasta zenye asili ya Italia hasa spaghetti.
[hariri] Tambi bichi na tambi kavu
Tambi zinaweza kutengenezwa jikoni na kupikwa zikiwa bichi. Lakini kwa kawaida huandaliwa kiwandani na kuuzwa ilhali zimekauka. Tambi kavu haziozi zinaweza kutunzwa kwa muda mrefu na zinapikwa haraka kwa muda wa dakika 8-15. Wachina waligundua njia za kutengeneza tambi zinazopikwa katika muda wa dakika 3 pekee.
[hariri] Tambi za nafaka na tambi za wanga nyingine
Aina nyingi za tambi hutengenezwa kwa kutumia unga wa nafaka kama vile ngano au mchele. Kuna pia aina zinazotumia wanga ya maharagwe, soya au viazi.
Tambi za kale kabisa zinazojulikana zimekutwa na wanaakiolojia nchini China kando la Mto Njano. Zina umri wa miaka 4,000 na zilitengenezwa kwa unga ya mtama.
[hariri] Aina za tambi
Kuna aina nyingi sana za tambi zinazotofautiana kwa umbo, rangi na ladha. Tabia hizi zinategemea na aina ya unga ambayo ni msingi wa tambi lakini pia na nyongeza kama vile mayai, mafuta, jibini na mengine ndani yake.
Aina za kimsingi ni pamoja
- Tambi za mayai hutengezenzwa kwa kutumia kinyunga cha unga ya ngano na mayai
- Tambi za ngano hutengezewa kwa kinyunga cha unga na maji pekee pamoja na chumvi
- Tambi za mchele hutengenezwa kwa unga ya mchele pamoja na maji
- tambi kioo hutengenezwa kwa kutumia wanga ya maharagwe au viazi; hazina rangi zinaonekana kama kioo
Kuna njia mbalimbali za upishi kwa mfano
- Tambi na mchuzi: tambi zinapikwa na kupelekwa mezani katika bakuli. Mchuzi wa majani, nyama au samaki huandaliwa kando na kumwagiliwa juu ya tambi kwenye sahani.
- Tambi katika supu: tambi zinapikwa katika supu pamoja na mboga majani, nyama na viungo vingine. Kama viungo huhitaji muda mrefu mpaka kuiva tambi zinaongezwa katika supu kwa dakika za mwisho
Makala hiyo kuhusu "Tambi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Tambi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |