Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Mwamba (jiolojia) - Wikipedia

Mwamba (jiolojia)

Kutoka Wikipedia

Graniti ni mwamba wa kivolkeno
Graniti ni mwamba wa kivolkeno

Mwamba katika jiolojia ni namna ya kutaja mawe au zaidi mchanganyiko wa madini ulio imara katika hali asilia. Jiwe ni kipande cha mwamba.

Takriban madini 30 hufanya sehemu kubwa ya miamba ya dunia ni hasa silikati na kabonati.

Yaliyomo

[hariri] Aina ya miamba

Mwamba hutokea kwa namna tatu:

  • mwamba wa mgando au mwamba wa kivolkeno unajitokeza pala ambako magma au lava inaganda.
  • mwamba mashapo hutokea pale ambako miamba inavunjika na kusagwa katika mmomonyoko na mashapo yanakandamizwa kwa njia ya kanieneo ya mashapo ya juu hadi mashapo kuwa mwamba mapya.
    • aina ya pekee ni mashapo yaliyosababishwa na wanyama au mimea itakayokuwa mwamba mashapo baadaye. Mfano: makaa mawe.
  • mwamba metamofia ni mageuzi ya miamba ya awali -ama ya kivolkeno au ya mishapo- kwa njia ya kanieneo kubwa sana na joto kali kuwa aina mpya ya mwamba. Metamofosi kwa kawaida hutokea katika kina kubwa.
Mzunguko wa miamba: 1 = magma au lava; 2 = kuganda kwa magma; 3 = mwamba wa kivolkeno; 4 = mmomonyoko; 5 = mashapo; 6 = mashapo + mwamba mashapo; 7 = mwendo wa gandunia, kuzama kwa mwamba na metamofosi; 8 = mwamba metamofia; 9 = kuyeyuka kwa mwamba ulio chini kwenye koti ya dunia kuwa magma mpya.
Mzunguko wa miamba: 1 = magma au lava; 2 = kuganda kwa magma; 3 = mwamba wa kivolkeno; 4 = mmomonyoko; 5 = mashapo; 6 = mashapo + mwamba mashapo; 7 = mwendo wa gandunia, kuzama kwa mwamba na metamofosi; 8 = mwamba metamofia; 9 = kuyeyuka kwa mwamba ulio chini kwenye koti ya dunia kuwa magma mpya.

[hariri] Mzunguko wa miamba

Miamba hubadilishwa umbo katika muda wa miaka mamilioni. Madini yao huingia katika hali mbalimbali ya mwamba.

  • a) Mwamba wa kivolkeno hutokea kwa kuganda kwa magma au lava.
  • b) Mwamba huu huvunjika kwa mmomonyoko na vipande vyake hubebwa na maji au upepo mahali vinapolala kama ganda la mashapo.
  • c) Mashapo kukandamizwa kwa njia ya kanieneo na kuwa mwamba mashapo.
  • d) Mwamba mashapo hufikia katika kina kubwa na kugeuzwa kwa njia ya metamofosi kuwa mwamba metamofia.
  • e) Hata hii mwamba metamofia husukumwa na nguvu za gandunia kufika tena juu na kupatwa na mmomonyoko kuwa mwamba mashapo.
  • f) Kila aina ya mwamba unaweza kumezwa na mwendo wa gandunia na kuyeyushwa tena kuwa magma.

[hariri] Meteori

Meteori ni mwamba wa pekee mwenye asili isiyo ya dunia yetu. Meteori nyingi zimejitokeza katika anga ya nje kutokana na mabaki ya mada ya nyota au pia kutokana na kuvunjika kwa sayari nyingine.

[hariri] Utamaduni

Mwamba ni muhimu katika utamaduni wa watu. Kihistoria vifaa vya kwanza vya kudumu vilikuwa vifaa vya mawe yaliyokatwa kuwa visu, shoka au nyundo. Wakati wa zama za mawe watu walikuwa hodari kutengeneza vifaa vya aina nyingi kutokana na mwamba.

Vilevile katika ujenzi mataifa mbalimbali yalitumia mwamba au mawe kwa majengo yao.

Mifano ya kale kabisa ya mwandiko ni mwandiko juu ya mwamba lakini kuna uwezekano ya kwamba watu walitumia pia ubao au kitu kingine lakini miandiko hii haikudumu na kutunzwa hadi leo.

Mawe ya thamani kama almasi hutafutwa na watu yakipendeza.


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -