Kosovo
Kutoka Wikipedia
Kosovo ( Kialbania: Kosovë au Kosova, Kiserbia kwa Kikirili: Косово и Метохија, Kiserbia kwa alfabeti ya Kilatini: Kosovo i Metohija) ni nchi ndogo ya Balkani katika Ulaya ya kusini-mashariki. Imepakana na Serbia, Jamhuri ya Masedonia, Albania na Montenegro. Mji mkuu ni Prishtina.
Kosovo ina wakazi milioni mbili. Takriban asilimia 88 ni Waalbania, 7 % Waserbia na wengine mchanganyiko wa Waturuki na vikundi vidogo. Waalbania wengi ni Waislamu wa dhehebu ya Sunni na Waserbia wengi ni Wakristo Waorthodoksi lakini kuna pia Waalbania Wakatoliki na Waorthodoksi pia Waserbia Waislamu kadhaa.
Yaliyomo |
[hariri] Uhuru usioeleweka
Kosovo ilikuwa sehemu ya Serbia hadi Februari 2008 ikatangaza uhuru wake tar. 17 Februari 2008. Jumuiya ya kimataifa haina msimamo wa pamoja juu ya uhuru wa nchi. Serbia inadai Kosovo bado ni jimbo lake la kujitawala. Nchi 37 pamoja na nchi nyingi za G8, Uturuki, Austria na Uswisi zimetambua Kosovo hadi Aprili 2008 na nchi mbalimbali zimetangaza kuwa zitafuata. Lakini nchi nyingine pamoja na Urusi, Jamhuri ya Watu wa China, Hispania na Serbia zinakataa.
Hali halisi tangazo la uhuru liliwezeshwa na maungano ya NATO ambayo imetawala Kosovo kwa niaba ya Umoja wa Mataifa. Jeshi la NATO lilizuia serikali ya Serbia lisingie kati kwa nguvu.
[hariri] Historia
Kihistoria Kosovo iliwahi kuwa eneo ambako ufalme wa kwanza wa Serbia ilianzishwa wakati wa karne ya 12. Hivyo Kosovo ilikuwa kitovu cha Serbia hadi mwisho wa milki ya Serbia ya Kale iliyovamiwa na Waturuki wa Milki ya Osmani.
Chini ya utawala wa Waturuki idadi ya Waserbia ilipungua kwa sababu wengi walikimbia ukandamizi wa Waosmani dhidi ya Wakristo. Waalbania walihamia humo kutoka maeneo ya jirani yaliyokuwa pia sehemu ya Milki ya Osmani. Katika karne ya 19 idadi kubwa ya wakazi wa Kosovo ilikuwa tayari Waalbania
[hariri] Utangulizi wa uhuru
[hariri] Kosovo ndani ya Yugoslavia
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Kosovo ilikuwa sehemu ya Jamhuri ya Serbia ndani ya shirikisho la Yugoslavia. Tofauti na sehemu kubwa ya Serbia inayokaliwa na Waserbia hasa wakazi wengi wa Kosovo ni Waalbania waliokuwa takriban robo tatu ya watu wote wa Kosovo hadi 1990. Hali halisi ilikuwa na haki za jamhuri ndani ya shirikisho lakini kutokana na uhusiano wa kihistoria haikupewa hadhi ya jamhuri kamili. Wakati wa kufarakana kwa Yugoslavia viongozi wa Serbia walifuta hali ya kujitawala ya Kosovo na kuwaachisha kazi maafisa wengi wenye utamaduni wa Kialbania.
Hii ilisababisha kipindi cha upinzani na ghasia ndani ya Kosovo kwa haki za Waalbania zilizokandamizwa na polisi na jeshi la Serbia. Amani ya Dayton ya 1995 juu ya sehemu zilizokuwa Yugoslavia haikuangalia maswali ya Kosovo. Hapa tangu 1996 vikundi kadhaa vya Kialbania vilianza kuchukua silaha na kupigania uhuru kwa njia ya kijeshi. Jeshi la Serbia ikajibu vikali na watu raia mamia waliuawa.
[hariri] Vita ya Kosovo
Mwaka 1999 wakimbizi wengi kutoka Kosovo walitafuta kimbilio katika nchi jirani na Umoja wa Ulaya. Baada ya majadiliano juu ya usuluhisho kushindwa NATO iliamua kungilia kati kwa kusudi la kuzuia kuongezeka kwa wakimbizi na mauaji na tar. 24 Machi 1999 ndege za kivia vilianza kushambulia madaraja, barabara, vituo vya umeme na taasisi za kijeshi katika Serbia. Jeshi la Serbia likaongeza kempeni yake katika Kosovo na idadi ya wakimbizi ikaongezeka.
Baada ya NATO kutisha uvamizi wa Kosovo kwa jeshi la ardhi serikali ya Serbia ilikubali tar. 12. Juni 1999 mapatano ya kuwa Umoja wa Mataifa kuchukua mamalaka juu ya Kosovo ikisaidiwa na NATO. Tar. 10 Juni 1999 Baraza la Usalama la UM lilimwagiza Katibu Mkuu kwa azimio 1244 kuanzisha utawala juu ya Kosovo. Hatua hii iliunda nchi lindwa chini ya UM na jeshi la NATO ambayo kisheria iliendelea kuitwa mkoa wa Serbia.
Ndani ya Kosovo NATO haikufaulu kuzuia matendo ya fujo na ghasia zilizolengwa dhidi ya wakazi Waserbia wa jimbo. Waserbia walipaswa kukimbia kutoka sehemu nyingi na wilaya mbili tu zilibaki kama maeneo ya Waserbia ndani ya Kosovo.
[hariri] Uhuru
Tar. 17 Februari 2008 bunge la Kosovo likatoa azimio la kutangaza uhuru wa nchi.
[hariri] Viungo vya Nje
- History of Kosovo and Metohija
- The Rastko Project
- Coordination Center of SCG and the Republic of Serbia for Kosovo
- Eastern Orthodox Resource Centre
- Southern Serbia: The second Kosovo?
- Hugo Roth, Kosovo Origins: an historian's comprehensive overview
Makala hiyo kuhusu "Kosovo" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kosovo kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |