Katharine Drexel
Kutoka Wikipedia
Katharine Marie Drexel (26 Novemba, 1858 – 3 Machi, 1955) alikuwa mtawa wa kike na mwanzishi wa jumuiya ya Masista wa Ekaristi Takatifu (kwa Kiingereza Sisters of the Blessed Sacrament). Jumuiya hiyo kwanza ililenga hasa kuwasaidia Wahindi Wekundu na Wamarekani Waafrika huko Marekani. Mwaka wa 2000 alitangazwa kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni 3 Machi.