Dresden
Kutoka Wikipedia
Dresden ni mji mkuu wa jimbo la Saksonia katika Ujerumani mwenye wakazi 484,700. Uko kando la mto Elbe.
[hariri] Historia
Dresden ilikuwa mji muhimu kama makao makuu ya wafalme wa Saksonia waliojenga jumba la kifalme na makanisa mazuri.
Mwishoni wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mji ukaharibiwa kabisa katika mashambulio ya jeshi la anga la Uingereza yanayojulikana kama maangamizi ya Dresden. Mji ulijaa wakimbizi kutoka sehemu za mashariki ya Ujerumani na takriban watu 35,000 walikufa katika siku tatu kati ya 13 na 15 Februari 1945.
Makala hiyo kuhusu "Dresden" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Dresden kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |