Kutoka Wikipedia
Ingawa jina langu rasmi ni Oliver Stegen, hapa Afrika Mashariki mimi huitwa Baba Tabita kwa ajili ya mtoto wa kwanza, binti anayeitwa Tabita.
Nimetoka Ujerumani lakini nimekaa Afrika Mashariki tangu mwaka wa 1996. Nafanya kazi kama mshauri wa kiisimu, na lengo langu ni kukuza matumizi ya lugha za Tanzania. Ndiyo sababu kuu ya kujitahidi kwangu upande wa ujenzi wa Wikipedia ya Kiswahili.
Hadi Desemba 31, 2007, nimetoa michango zaidi ya elfu kumi na tano (15,000).
Ingawa nimechaguliwa kuwa bureaucrat wa wikipedia hii mwezi wa pili 2008, kazi yangu hunisafirisha mara kwa mara kwenda maeneo ambako hakuna mtandao hata kidogo. Nikiwa kimya kwa majuma kadhaa, naomba mnivumilie. Asanteni!