Sinagogi
Kutoka Wikipedia
Sinagogi ni nyumba ya kusali ya Wayahudi.
Yaliyomo |
[hariri] Etimolojia
Neno latokana na Kigiriki συναγωγή sinagoge likimaanisha "mkutano"; ni tafsiri ya Kiebrania בית כנסת beit knesset yaani "nyumba ya mkutano". Wayahudi hutumia pia neno la Kiyiddish "shul" (=shule) kwa sinagogi.
[hariri] Muundo
Chumba kikuu ni ukumbi wa sala na mara nyingi kipo pamoja na vyumba vya pembeni kama vile madarasa, ofisi na vingine.
[hariri] Historia
Katika Israeli ya Kale kabla ya uvamizi wa Yerusalemu mwaka 587 KK hapakuwa na sinagogi wala hazitajwi kabisa katika Agano la Kale.
Hakuna uhakika kamili lakini inaonekana ya kwamba sinagogi zilianzishwa baada ya kubomolewa kwa hekalu ya Yerusalemu na uhamisho wa Wayahudi katika nchi za mbali.
Tangu kuharibiwa wa Hekalu ya Pili mwaka 70 Wayahudi walikuwa na masinagogi tu.
[hariri] Yaliyomo
Ukumbi wa sala huwa na sehemu zifuatazo:
- sanduku la Torati ni kabati au sanduku ambako hati za kuviringisha zenye mwandiko wa Biblia hutunzwa.
- taa inayoendelea kuwaka muda wote
- meza ya msomaji ambako hati za torati hufunguliwa na kusomewa
- mimbari ya mafundisho
- kinara cha menorah chenye mishumaa 7 au 9
Makala hiyo kuhusu "Sinagogi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Sinagogi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |