Ramani
Kutoka Wikipedia
Ramani ni picha -kwa awaida mchoro- ya dunia au sehemu au sifa zake. Ni tofauti na picha iliyopigwa kwa kamera kutoka ndege au chombo cha angani kwa sababu mchora ramani anaamua anachotaka kuonyesha na kuzipa uzito sifa anazotaka kuweka mkazo.
Kuna aina nyingi za ramani.
- ramani za topografia huonyesha uso wa dunia (kwa mfano: bahari, nchi, milima, mito, kimo cha ardhi na kina cha bahari)
- ramani za sifa huonyesha sifa fulani kuhusiana na dunia (kwa mfano: historia, uchumi, usambazaji wa wakazi katika nchi n.k.)
- ramani inaweza kufuata uso wa dunia
- ramani inaweza kufuata mahitaja ya mtazamaji (ramani ya njia ya reli huonyesha mstari tu na ufuatano wa vituo bila kutaja kona na mabadiliko ya mwelekeo)
Kila mchora ramani anahitaji kuamua jinsi ya kuonyesha mambo yake. Kwa ramani za kijiografia tatizo hutokana na umbo la dunia ambayo ni tufe wakati ramani kwa kawaida ni karatasi bapa.
xc:Tamil
Makala hiyo kuhusu "Ramani" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Ramani kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |