Pieter Brueghel Mzee
Kutoka Wikipedia
Pieter Brueghel (* kati ya 1525 na 1530 mjini Breda; † 5 Septemba 1569 Brussels) alikuwa mchoraji Mholanzi wa karne ya 16. Anaitwa "Brueghel Mzee" ili kumtofautisha na mwanawe Pieter Brueghel Kijana aliyekuwa mchoraji mashuhuri pia. Anahesabiwa kati ya wachoraji muhimu zaidi wa Zama ya Mwangaza ya Ulaya.
Brueghel alijifunza sanaa ya uchoraji mjini Antwerpen hadi kufikia kiwango cha fundi mwalimu. Mnamo 1552-1555 alisafiri Italia alikoangalia sanaa ya karne nyingi.
Picha za Brueghel zinaonyesha vinaganaga vingi alipenda kuficha ujumbe wake katika vipengele vidogo. Alipenda kuonyesha maisha ya wakulima vijijini kwa umakini kabisa. Picha zake zote zinasimulia hadithi katika mazingira ya mandhari ya kiholanzi. Alichora pia habari za Biblia na ndoto akifanana na Hieronymus Bosch.
Kati ya picha zake mashuhuri sana ni "Misemo na nahau za lugha ya Kiholanzi" alimoonyesha misemo zaidi ya 100, halafu pia "Mnara wa Babeli".
[hariri] Viungo vya Nje
- Biography at the Web Gallery of Art
- Web Gallery of Art: Paintings by Pieter Bruegel the Elder
- Pieter Bruegel the Elder at Olga's Gallery
- Pieter Bruegel the Elder in the "A World History of Art"
- Complete list of paintings. Includes all of the 100 proverbs from the painting, with explanation (in French).
- www.all-art.org/early_renaissance About Pieter Brueghel the Elder
- Timken Museum of Art's "Parable of the Sower" by Pieter Bruegel the Elder