Nakamikado
Kutoka Wikipedia
Nakamikado (14 Januari, 1702 – 10 Mei, 1737) alikuwa mfalme mkuu wa 114 (Tenno) wa Japani. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Yasuhito. Tarehe 27 Julai, 1709 alimfuata baba yake, Higashiyama, na kuwa mfalme hadi kujiuzulu tarehe 13 Aprili, 1735. Aliyemfuata ni mwana wake, Sakuramachi.