MGIMO
Kutoka Wikipedia
Chuo Kikuu cha Moskva cha Mahusiano ya Kimataifa cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi (Kirusi: Московский государственный институт международных отношений (Университет) МИД России MGIMO MID) ni chuo kikuu kimojawapo mjini Moskva katika Urusi.
Kimeanzishwa mwaka 1943 kikiwa ni kitivo cha Chuo Kikuu cha Taifa cha Moskva (Moscow State University - MSU), mwaka 1944 kikapata hadhi ya chuo kikuu.
Kwa sasa zaidi ya wanafunzi 4500 wanasoma huko, wakiwemo wageni. Jumla ya vitivo ni 12. Masomo yanayopewa ni pamoja na udiplomasia, uchumi wa dunia, uandishi habari, utembezi, sheria ya kimataifa n.k.
[hariri] Viungo vya Nje
- Tovuti rasmi: http://www.mgimo.ru
- Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi:
Makala hiyo kuhusu "MGIMO" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu MGIMO kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |