Mangosuthu Buthelezi
Kutoka Wikipedia
Inkosi Mangosuthu ("Gatsha") Ashpenaz Nathan Buthelezi (amezaliwa tar. 27 Agosti, 1928) ni kiongozi wa Kizulu huko nchini Afrika Kusini, na vile vile kiongozi wa chama cha Inkatha Freedom Party (IFP) ambacho kiliundwa mwaka 1975.
Yaliyomo |
[hariri] Wasifu
[hariri] Maisha ya awali
Mangosuthu alizaliwa mnamo tar. 27 Agosti mwaka wa 1928, mjini Mahlabathini, KwaZulu-Natal, na Chief Mathole Buthelezi na binti wa mfalme Magogo kaDinizulu, ambaye ni dada wa mfalme Solomon kaDinuzulu. Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Impumalanga iliyoko Mahashini, Nongoma, tangu mwaka 1933 hadi mwaka 1943, kisha katika chuo kimoja kiitwacho Adams College, kilichopo Amanzimtoti, tangu mwaka 1944 hadi 1947.
Baadae akaelekea katika Chuo Kikuu cha Fort Hare kuanzia mwaka 1948 hadi 1950, ambapo huko ndiko aliko jiunga na chama cha African National Congress Youth League na kuanza kupata mawasiliano na Robert Mugabe na Robert Sobukwe. Mangosuthu alifukuzwa Chuoni baada ya wanafunzi kuleta mgomo. Kisha baadae alikuja kumalizia Digrii yake katika Chuo Kikuu cha Natal.
[hariri] Marejeo
- William Beinart, "Twentieth Century South Africa", Oxford, 2001, pg. 330
[hariri] Viungo vya nje
- Wasifu kuhusu Buthelezi
- Habari zinazo jadili kuhusu kupigwa chini kwa Buthelezi kuwa kama Waziri mkuu wa mambo ya ndani
- Chief Mangosuthu Gatsha Buthelezi
- Asili ya kabila la Buthelezi
- [1]
- [2]