Kizulu
Kutoka Wikipedia
Kizulu (isiZulu) ni lugha ya Wazulu inayoongelewa nchini Afrika Kusini na idadi ya watu wanaokadiriwa kuwa milioni 9-10 hasa katika jimbo la KwaZulu-Natal. Kizulu huhesabiwa kati ya lugha za Kinguni ndani ya lugha za Kibantu.
Wakati wa mfecane katika karne ya 19 wasemaji wa lugha ya Kizulu zimehama hadi Zimbabwe, Zambia, Msumbiji na Tanzania ambako lugha imebadilika kiasi kuwa kwa mfano Kindebele au Kingoni.
Makala hiyo kuhusu "Kizulu" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kizulu kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |