James Dewey Watson
Kutoka Wikipedia
James Dewey Watson (amezaliwa 6 Aprili, 1928) alikuwa mwanafizikia wa biolojia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza virusi na mfumo wa molekuli mbalimbali, hasa DNA. Mwaka wa 1962, pamoja na Francis Crick na Maurice Wilkins alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
Mwaka 2007 alijikuta katikati ya ugomvi kuhusu mahojiano aliporipotiwa kusema ya kuwa watu wa rangi nyeusi hawana akili sasa na Wazungu. Baadaye Watson karudi nyuma akieleza ya kwamba hakumaanisha alichosema.