Chicago
Kutoka Wikipedia
Chicago ni mji mkuu wa wa jimbo la Illinois na pia mji mkubwa wa tatu nchini Marekani. Iko kando ya Ziwa Michigan. Idadi ya wakazi ni 2,900,000 (2000) na pamoja na rundiko la mji ni watu milioni tisa.
Ni mji muhimu wa biashara na viwanda. Kwa kuwa meli za Atlantiki zinafika Chicago kupitia njia ya maji ya Saint Lawrence na pia ni chanzo cha reli muhimu huitwa mara nyingi "geti ya magharibi" ya Marekani. Kabla ya kujengwa kwa reli mfereji muhimu uliunganisha mji na mto Mississippi.
Chanzo cha Chicago kilikuwa kituo cha biashara kwenye mdomo wa mto Chicago. Mji uliundwa 12 Agosti 1833 ukawa manisipaa 1837. Wakazi waliongezeka haraka. Walikuwa 30,000 mwaka 1850, 100,000 mwaka 1860 na hadi 1880 waliongezeka kuwa 500,000. Milioni ilifikwa 1890.
Kwa miaka mingi jengo la Sears Tower lilikuwa nyumba kubwa ya dunia kati ya 1974 hadi 1998 ikiwa na kimo cha mita 442.